Wanajeshi wa Israel wamewapiga risasi na kuwaua watu watatu waliokuwa na silaha kali ambao walipenya mpaka wa Misri kisirisiri na kuwavizia wanajeshi leo, ili kuepusha "shambulio kubwa sana la kigaidi," msemaji wa jeshi alisema, kulingana na Agence France-Presse.
Mwanajeshi wa Israel pia aliuawa katika mapigano hayo ya moto, Reuters iliripoti.
"Walifyatua risasi kuelekea askari wa IDF [Jeshi la Ulinzi la Israel] waliokuwa wakiwalinda wafanyakazi [waliokuwa wakijenga uzio] katika eneo hilo. Kikosi kingine kilichokuwa karibu… kilikimbia hadi eneo hilo na kuwalenga wale magaidi watatu,” alisema msemaji Luteni Kanali Avital Leibovich, akisema wote watatu waliuawa.
Septemba/21/2012


