Jeshi lilisema katika taarifa yake kwamba wanajeshi wa serikali walilenga maficho ya waasi katika maeneo ya Bustan al-Qasr, Bustan al-Basha na al-Sheikh Khudr, na kuua idadi ya "magaidi" hapo Jumamosi.
Imeongeza kuwa jeshi pia limeharibu idadi ya magari ya waasi wakati wa operesheni tofauti katika vitongoji vitatu vya Aleppo.
Jeshi la Syria limekuwa likiongeza juhudi zake za kuwaondoa waasi katika vitongoji zaidi vya Aleppo wanaopambana na vikosi vya serikali.
Syria imekuwa ikikumbwa na machafuko tangu Machi 2011. Damascus inasema 'waharibifu, wavamizi, na magaidi wenye silaha' ndio chanzo cha machafuko na ghasia mbaya huku upinzani ukishutumu vikosi vya usalama kwa kuhusika na mauaji hayo.
Mataifa ya Magharibi yamekuwa yakimtaka Rais Bashar al-Assad wa Syria aondoke madarakani. Hata hivyo, Urusi na China zinapinga vikali dhamira ya nchi za Magharibi ya kumng'oa Assad madarakani.
Serikali ya Syria inasema machafuko hayo yanapangwa kutoka nje ya nchi, na kuna ripoti kwamba idadi kubwa sana ya wapiganaji wenye silaha ni raia wa kigeni, wengi wao kutoka Misri, Algeria, Saudi Arabia na Afghanistan.
(Bonyeza TV)


