Hoja hiyo iliyosasishwa Alhamisi, inaidhinisha serikali ya Uturuki "kutuma wanajeshi wa Uturuki, kwa lengo la kumaliza vitisho vya ugaidi na mashambulizi, katika operesheni za mpakani katika eneo la kaskazini mwa Iraq ambako PKK imejenga kiota,” Reuters iliripoti.
Hoja hiyo ilipitishwa kwa mara ya kwanza mnamo 2007.
Mapema mwezi huu, Iraq ilitoa wito wa kukomesha uwepo wa vikosi vya jeshi la Uturuki katika ardhi yake, na kuitaka Uturuki kusitisha mashambulizi yake dhidi ya PKK.
Katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita, wanajeshi wa Uturuki na PKK wamehusika katika moja ya mapigano makali zaidi tangu kuanza kwa mapambano ya silaha ya kundi la wakurdi dhidi ya Ankara.
Mwezi Julai, Baghdad aliionya Ankara dhidi ya "ukiukaji" wa ardhi yake na anga na ndege za kivita za Uturuki na kuitaka Wizara yake ya Mambo ya Nje kuwasilisha malalamiko yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala hilo.
Kundi la PKK limekuwa likipigania taifa huru kusini magharibi mwa Uturuki tangu miaka ya 1980.
Tangu miaka ya 1990, Uturuki imedumisha kambi kadhaa za kijeshi katika eneo la Kurdistan kaskazini mwa Iraq ambapo PKK pia imeweka kambi za nje.
Kambi moja ya kijeshi ya Uturuki iko katika eneo la Bamerni katika mkoa wa Dohuk, mojawapo ya majimbo matatu yanayounda eneo la Kurdistan. Uturuki pia ina kambi tatu za kudumu za kijeshi huko Kani Massi, Dera Luk na Sirsi ambapo hutuma wanajeshi mwaka mzima.
Mzozo wa Ankara-PKK umesababisha vifo vya zaidi ya watu 45,000.


